Nifanye
nini nipate kuokokolewa
“Nifanye
nini nipate kuoko lewa?” Hili
ndilo swali la muhimu kuliko yote ambayo kamwe tutawahi kuuliza – jibu lake ni
la muhimu vivyo hivyo. Tukitaka kwenda mbinguni ni muhimu tuhakikishe kuwa
tunajua kuwa jibu sahihi ni lipi. Matokeo ya kutokulijua jibu sahihi ni
yanatisha, hata kwa kule kuyafikiria tu. Matokeo yake ni kuishia kuteseka
milele huko Jehanam.
_______________
BIBLIA Ni NENO LA MUNGU
Kuna vitabu vingi
vizuri vilivyoandikwa lakini kitabu kimoja kimesimama juu ya vyote. Ni kitabu
ambacho Mungu anaongea na mwanadamu nacho ni Biblia. Vitabu vingine vimeandikwa
na wanaume na wanawake wenye akili sana, lakini Biblia ni tofauti , mwandishi
wa Biblia ni Mungu.
___________________________________
KANISA
MOJA
moja
kanisa - mwili - misheni
Leo
ukitazama kila mahali, kuna makanisa mengi sana. Inachanganya sana tunapofikiri
kuhusu jambo hilo. Makanisa mengi sana, kila moja na mafundisho yake na kila
moja likifundisha mambo tofauti. Yanatueleza njia tofauti za kumwabudu Mungu,
yanatupa maelekezo ya jinsi ya kuishi. Vile vile yanatufundisha njia mbalimbali
za kuokolewa.
Hakika
hili siyo sahihi! Tunamtumikia Mungu mmoja na tunaye mwokozi mmoja, Yesu
Kristo.
KANISA MOJA
No comments:
Post a Comment